Gilbert Ongaki Manyura

Mhadhiri
Mhadhiri wa Kiswahili katika Chuo Kikuu cha The East African University, Kitengela
Biografia
Naitwa Bw. Gilbert Ongaki Manyura. Mimi ni mhadhiri wa Kiswahili katika Chuo Kikuu cha The East African University, Kitengela. Nilihitimu Siasa, Dini na Kiswahili kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi. Baada ya kuwa mwalimu wa shule za sekondari, nilijiunga katika Chuo Kikuu cha Egerton ambapo nilifuzu shahada ya uzamili katika Kiswahili. Kwa sasa, nimo katika harakati za kukamilisha shahada ya uzamifu katika Kiswahili kutoka Chuo Kikuu cha Kisii.
Ningependa kuchukua fursa hii kuwakaribisha wakazi wa Kajiado, Kenya yote na jumuiya ya Afrika Mashariki kwa jumla ambao wangependa kuendeleza masomo yao ya juu kuchagua chuo chetu katika azma hii.
Chuo chetu kina mazingira murua kwa yeyote anayenuia kufanikisha ndoto yake ya kielimu. Kuna nafasi kuanzia kiwango cha cheti, stashahada, ukapera, uzamili hadi uzamifu.
Katika Kiswahili, hatuandai wanafunzi wetu kuwa walimu tu, bali pia huwapa maarifa ya kuwa wachambuzi na wahakiki, watafsiri, waandishi wa vitabu, waandishi na wasomaji habari, kando na taaluma nyingine nyingi.
Wahadhiri wamehitimu vizuri na wako tayari kunoa wanafunzi kitaaluma, ili kuthibitisha kilichosemwa na wahenga kuwa cha mkufuu mwanafuu ha na akila hu.
Aidha, kuna kozi fupifupi za kuimarisha hadhi ya mwanafunzi maishani. Miongoni mwazo ni lugha za kimataifa kama vile Kijerumani, Kichina, Kifaransa na Kiarabu.